- Votes:
Malika - Kama Zamani lyrics
Wangu muibaka, sikuezi sikuoni
Tangu kuondoka, moyo umo msibani
Sijui hakika ilokuudhi ni nini
Naombathe mkaa unijaze kwa makini
Chorus:
Mimi nakutaka mimi nakutaka
Mimi nakutaka, Sijui wewe unani?
Wewe unani? Wewe unani?
Nakutaka (Wewe) Nakupenda (Wewe)
Nakutaka (Wewe) Nakupenda (Wewe)
Sijashiba na bado nakuthamani
Laniadhibu pendo lako fulani
Fanya kulahali, Fanya kulahali
Fanya kulahali, Urudi kama zamani
Kama zamani, Kama zamani,
Nyonda fanya hima, usichelewe haraka
Ingiwa huruma, juwa mimi nakutaka
Usiniweke nyuma, kwa mapenzi nateseka
Tuishi daima, kwa kusema na kutheka
Malika - Kama Zamani - http://motolyrics.com/malika/kama-zamani-lyrics.html
(Chorus)
Naona udhiya, wewe kuwa nami mbali
Yangu mazoeya, kabisa kutoa ya ajali
Hebu fikiria moyo ni zidi thakili
Bwana niridhiya, nitunze yangu akili
(Chorus)
Sitotia toba, kukuatha duniani
Bado sijashiba, nakuaza muhisani
Nazitaka hoba, mwenziyo nimaraghini
Nipe zako tiba, utunze kwa makini
(Chorus)
Makosa nirudi, ikiwa ni makosani
Siwe mkaidi, kweli yako ubaini
Ziweke baidhi, maudhi futa moyoni
Na kwangu urudi, kama hali ya zamani
(Chorus)